Thursday, March 24, 2011

FAMILIYA YA BURUDANI HASA MUZIKI WA TAARABU IMEPATA PIGO


FAMILIA ya burudani hasa muziki wa taarab imepata pigo baada ya wanamuziki wa Kundi la Five Stars Modern Taarab, kupoteza nyota wake 13 kwa wakati mmoja katika ajali iliyohusisha magari matatu katika eneo la Mikumi mkoani Morogoro. ambayo ni malori mawili na basi dogo aina ya Coaster lililokuwa limewabeba wasanii hao likitokea Kyela, Mbeya.


Ajali hiyo ilitokea majira ya saa 2:30 usiku wakati gari aina ya Coaster lenye namba za usajili T351 BGE likitokea Kyela Mbeya, lilitaka kulipita lori lenye namba za usajili T848 ATE, lakini jaribio hilo lilishindikana baada ya kukutaka na lori lingine lenye namba za usajili T530 BHY hivyo kurejea kwenye usawa wake na kulivaa lori hilo ambapo mbao ziliwaumiza na kuwaua wasanii wa kundi hilo la Five Star Modern Taarab  waliokuwepo kwenye Coaster hiyo.


Tukio hilo lilisababisha wasanii 12 kupoteza maisha hapo hapo. Mmoja alifariki dunia wakati akipatiwa matibabu. Kwa upande wa hali za marehemu, wengi wao miili imeharibika sana, imehifadhiwa kwenye hospitali ya mkoa wa Morogoro.  Miili hiyo itarajia kuwasili jana mchana kwa ajili ya shughuli za mazishi.


Waliofariki:
Nassor Madenge
Issa Ally ‘Kijoty’
Shebe Juma
Omar Hashim
Tizo Mapunda
Omar Tall
Ngereza Hassan. 

Wengine ni Husna Mapunda, Maimuna, Haji Mzamila na mmoja aliyefahamika jina moja la Haji huku mwanaume 
mwingine hakutambulika jina lake mara moja.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.