Saturday, January 29, 2011

MWANAFUNZI aliyeongoza mtihani wa kidato cha nne kitaifa mwaka 2010


 Lucylight Mallya (18), amebainika kuwa ni yatima ambaye wazazi wake wote walifariki dunia miaka minne iliyopita.

 Lucylight alizaliwa Jijini Dar es Salaam, miaka 18 iliyopita alisoma Shule ya Msingi St Mary's Tabata na baada ya  alihitimu la saba mwaka 2006 alichaguliwa kwenda Shule ya Sekondari ya Wasichana Tabora lakini aliamua kwenda Marian Girls alikohitimu kidato cha nne mwaka jana.
 
Taarifa za maendeleo yake zinaonyesha kuwa akiwa kidato cha kwanza alishika nafasi ya tatu, lakini kuanzia kidato cha pili hadi cha nne alikuwa akishika nafasi ya kwanza.

Lucylight anaishi na Baba Mkubwa wake kijiji cha Nduruma wilayani Arumeru, ambaye anaitwa Dominick Mallya.
  
Lucylighty ambaye ni kwanza kati ya watoto, wanne walioachwa na marehemu wazazi walofariki dunia mwaka 2006 na (2007),  malengo yake ni kuwa daktari.
 
Binti huyu amesoma katika mazingira magumu kwasababu hakuwa na fedha za kutosha
  
Hata hivyo, aliomba wafadhili wa kumsaidia, ili aweze kuendelea ya masomo ya kidato cha tano hadi sita na chuo kikuu kwasababu Baba Mkubwa wake (Mallya) hana fedha za kutosha kuwasomesha watoto wote alionao.
 
Baba yake Lucy ambaye ni  alifariki dunia mwaka 2006  na mkewe alifariki mwaka 2007, waliacha watoto wane.
 

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.