Monday, April 2, 2012

Thursday, March 22, 2012

MWANRY, Nchemba,Sioi na mkewe Sioi, Pamella, wakicheza wakati wa mkutano wa kampeni KIA.




MJUMBE wa NEC ya CCM na Mbunge wa Siha, Aggrey Mwanri, akihutubia mkutano wa kumnadi mgombe wa CCM, Sioi sumari, KIA.



WANANCHI wa Kijiji cha Mareu, wakimhakikishia Sioi wanampigia kura Aprili Mosi mwaka huu kuwa mbunge wao.



SIOI, akipokewa na kinamama alipowasili katika kijiji cha Mareu kuhutubia mkutano wa kampeni.





SIOI (wa nne kushoto),akiwa na viongozi wengine wa CCM, wakitoa heshima kwenye kaburi la aliyekuwa Katibu wa CCM wa kata ya King'ori, Marehemu Aminiel Nnko aliyefariki kwa ajali ya gari wiki iliyopita



MGOMBEA Ubunge wa CCM katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Arumeru Mashariki, Sioi Sumari, akisalimiana na wanafunzi wa Shule ya Msingi Upendo iliyoko kijiji cha Ngejisosia.

MBUNGE wa Viti Maaalumu kupita Umoja wa Vijana wa CCm, Ester Bulaya, akihutubia mkutano wa kampeni katika kijiji cha Ngejisosia.

PICHA ZA MATUKIO YA KAMPENI YA CCM ARUSHA KWENYE JIMBO LA ARUMERU MASHARIKI

Mgombea huyo akinadiwa na Mwenyekiti wa Jimbo wa chama hicho, Elias Matoto (kulia) katika mkutano huo wa uzinduzi wa kampeni za SAU kwenye viwanja vilivyopo eneo la Majani ya Chai jimboni Arumeru Mashariki. Kushoto ni Meneja wa kampeni za SAU Johnson Mwangozi



SAU KUZINDUA KAMPENI ZAKE . JIMBO LA ARUMERU MASHARIKI MKOA WA ARUSHA



Saturday, October 22, 2011

AJALI YA NDEGE MKOANI ARUSHA

RUBANI wa ndege ndogo aina ya Piper Pa 34- 300 namba 5H-QTE, mali ya World Quality
Travel and Tour Limited, Ally Harun (24), mkazi wa Arusha, amekufa huku rubani msaidizi
Lilian Koima, akijeruhiwa na kukimbizwa katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC Kilimanjaro, baada ya ndege hiyo kuanguka Arumeru.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Akili Mpwapwa, alisema ndege hiyo ilikuwa na marubani wawili ambao ni marehemu na mwenzake Lilian Koima, ambaye hajajulikana umri wake na makazi yake, wakitokea Dar es
Salaam na kuelekea uwanja wa ndege wa Arusha.

Alisema ndege hiyo ikiwa angani saa 1.46 usiku na ikiwa imekaribia uwanja wa Arusha kutua, ilishindwa kutua kwa sababu ya giza nene kutanda uwanjani hapo na kulazimika kubaki angani.

“Wakati wakiwa angani mmoja wa rubani hawa akapiga simu Tower Control wa Uwanja wa (KIA) na kuomba kutua huko, nao aliwaruhusu na wakiwa njiani kuelekea huko, ilianguka katika kijiji cha Samaria kata ya Kikatiti, Arumeru na mawasiliano yakakatika ghafla kati yao na KIA,” alisema Mpwapwa.

Alisema ndege hiyo ilianguka karibu na nyumba ya Maria Akyoo na kuharibika na kuua mbuzi watatu walioangukiwa papo hapo, pia kibanda cha biashara kiliharibiwa.

Kamanda Mpwapwa alisema Ally alikufa papo hapo huku Lilian akijeruhiwa na kukimbizwa KCMC. Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Mkoa ya Mount Meru.

Alisema chanzo cha ajali hiyo bado hakijajulikana na Polisi inaendelea na uchunguzi. Meneja wa Uwanja wa Ndege wa Arusha, Simon Kimiti, alisema kwa njia ya simu kuwa hatakiwi kujibu lolote na anayetakiwa kuzungumzia suala hilo ni watu wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa
Kilimanjaro - KIA.

Taarifa ya Wizara ya Uchukuzi iliyotolewa jana ilisema ndege hiyo yenye injini mbili na uwezo wa kubeba abiria sita ni mali ya Mawala Advocates na ilikuwa ikisafiri kutoka Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam kwenda Kilimanjaro.

Kwa mujibu wa Edward Mkiaru aliyesaini barua hiyo kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya
Uchukuzi, wakaguzi wa ajali za ndege kutoka Wizara hiyo wako Kilimanjaro kuchunguza chanzo cha ajali.

Wednesday, August 10, 2011

KONDOO MWENYE KORANI AZALIWA



KIJIJI cha Uduru wilayani Hai mkoani Kilimanjaro kimegeuka eneo la utalii baada ya waumini wa madhehebu ya Kiislamu kutoka maeneo mbalimbali wilayani humo na maeneo jirani, kwenda kumshuhudia kondoo aliyezaliwa ameandikwa maneno mwilini kwa lugha ya Kiarabu.

Waumini hao walifurika kijijini hapo juzi baada ya sala ya Ijumaa kumshuhudia kondoo huyo aliyezaliwa wiki tatu zilizopita na kuacha watu midomo wazi kutokana na kuwa na maandishi yanayosomeka kiarabu ubavuni, yakitafsiriwa kwa Kiswahili kama Yasini.

Kondoo huyo aliyezaliwa katika familia moja ya waumini wa dini ya Kikristo, aliwavuta
waumini wengi kijijini hapo na kutoka nje ya wilaya na mkoa wa Kilimanjaro kwa ajili ya kushuhudia tukio hilo la ajabu na la kihistoria ambalo halijawahi kutokea.

Grace Massawe (55) alisema kondoo huyo alizaliwa takribani wiki tatu zilizopita na hakuwahi kutambua kwamba beberu huyo alikuwa na maandishi hayo, kutokana na kutotolewa nje na mama yake.

Grace alisema baada ya kondoo huyo kuzaliwa, mama yake alibadilisha tabia na kukaa ndani ambapo awali alikuwa akila chakula nje na wenzake, lakini aligundua maandishi hayo baada ya kumtoa nje mwenyewe.

Alisema awali aliona herufi ya W yenye rangi ya dhahabu, lakini siku zilivyozidi kwenda neno hilo lilizidi kukua na kubadilika rangi na kuwa jeupe zaidi, hali iliyompa wasiwasi na kutafuta msaada ili kutambua maana ya maandishi hayo kutoka kwa waumini wa Kiislamu.

“Baada ya waumini wa Kiislamu kufika hapa nyumbani walibaini maandishi hayo ubavuni mwa kondoo huyo kuwa ya Kiarabu yanayosomeka kuwa Yasini,” alisema Grace.

Alisema waumini hao walimweleza kuwa neno hilo ni muhimu sana katika Kitabu Kitakatifu cha Korani, ambalo ni kama kitovu cha kitabu hicho, pia ni moja ya sura muhimu ndani ya kitabu hicho.

Katika hatua nyingine, Grace alisema katika ufugaji wake wa kondoo hakujawahi kutokea tukio la ajabu kama hilo na kueleza kuwa kondoo aliyemzaa alikuwa ni uzao wake wa mara ya pili ambapo awali alizaa kondoo wa kawaida.

Alisema kutokana na kondoo huyo kuvuta hisia za watu wengi, pia viongozi wakubwa wa dini hiyo walifika kushuhudia maajabu hayo, akiwamo Katibu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) wa Mkoa wa Kilimanjaro, Shehe Rashid Mallya, na Shehe Mkuu wa Wilaya ya Hai, Juma Lyimo.


Juhudi za kumtafuta Shehe Mallya kuzungumzia tukio hilo, zilishindikana baada ya simu yake kuita bila kupokewa.


Samaki wa Kupaka

Samaki wa Kupaka

Monday, May 16, 2011

VIJANA WA UMOJA WA VIJANA WA CHAMA CHA MAPINDUZI[UVCCM] WAKISHIRIKI KATIKA KUFANYA USAFI NA KUWAFARIJI WAGONJWA

PICHA SIKU YA KIMATAIFA YA FAMILIA


UMOJA WA VIJANA WA CHAMA CHA MAPINDUZI [UVCCM] UMESHIRIKI KATIKA KUFANYA USAFI NA KUWaFARIJI WAGONJWA KATIKA HOSPITALI KUU YA SERIKALI YA MKOA WA ARUSHA YA  MOUNT MERU IKIWA NI SEHEMU YA MAADHIMISHO YA SIKU YA KIMATAIFA YA FAMILIA,KUSHOTO MJUMBE WA BARAZA KUU LA TAIFA LA UMOJA HUO NA MBUNGE WA VITI MAALUMU CATHERIN MAGIGE AKIWA NA MMOJA YA WATOTO WALIOZALIWA KATIKA HOSPITALI HIYO NA KULIA NI MAKAMU MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA ARUSHA ANNA MSUYA